Kocha wa zamani wa club ya Arsenal ya England aliyokuwa akiifundisha tokea 1996 hadi 2018 alipoamua kujiuzulu nafasi hiyo kwa maslahi mapana ya club Arsene Wenger, aemfunguka na kuelezea mitazamo ya watu kuhusiana na staa wa Arsenal Mesut Ozil aliyomnasa wakati wa utawala wake Emirates.
Arsene Wenger ametoa kauli inayoashiria kumtetea Mesut Ozil ambaye amekuwa na wakati mgumu kisoka kwa sasa chini ya kocha mpya Unai Emery, Wenger anasema kumsajili mchezaji kwa miaka mingi kama Ozil haimaanishi kwamba atacheza kwa kiwango bora kwa muda wote ila ni kumuweka huru zaidi na kuonesha uwezo wake kwa ufasaha.
“Nafikiri urefu wa mikataba kwa mchezaji kwa kawaida hauna kitu cha kufanya katika kuchagua wachezaji wa kuanza, mara nyingi tunafikiri tunapokuwa tumemsajili mchezaji kwa miaka mitano kwamba tutakuwa na mchezaji mzuri kwa miaka yote mitano lakini haina maana hiyo, maana yake atacheza kwa ubora kwa sababu atakuwa yupo sehemu ya faraja”>>>Arsene Wenger
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Kocha Arsene Wenger alimsajili Mesut Ozil 2013 akitokea Real Madrid ya Hispania kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 42.5 lakini mwaka 2018 aliongeza mkataba wa kusalia Arsenal hadi 2021 uliyomfanya awe analipwa mshahara wa pound 350000, kwa sasa hayupo katika nafasi nzuri ndani ya Arsenal.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba