Pamoja na mambo ya kuzingatia kwa wanaotumia huduma za fedha kwa simu, wanaofanya biashara kwenye mitandao au biashara na shughuli zinazohusiana na simu wanashauriwa kuzingatia yafuatayo:
1. Kujisajili kwa mtoa huduma husika kwa kutumia taarifa zako binafsi na kuepuka kutumia taarifa au vibali vya watu wengine.
2. Kuwa makini dhidi ya wahalifu. Kwa vile biashara hizi zinahusisha mzunguko mkubwa wa
fedha, zinalengwa na wezi mtandaoni na wale wa kawaida.
3. Kuhakikisha kwamba simu inayotumika kwa miamala ya kifedha ni tofauti na inayotumika
kwa shughuli nyingine na kuhakikisha simu hiyo haitumiwi na mtu mwingine. Vilevile waagize
wahudumu wako wasipokee maagizo ya mtu mwingine kuhusiana na biashara yako. Maelekezo
yote lazima yafanyike uso-kwa-uso, au kwa njia ya simu ya maongezi tu.
4. Tumia namba ya siri ambayo sio rahisi mtu mwingine kukisia. Ni hatari na uzembe kutumia
mwaka wa kuzaliwa kama namba ya siri, kwani ni rahisi kukisiwa.
5. Iwapo unauza laini za simu, hakikisha unasajili wanaonunua kwa kutumia vitambulisho vyao halisi vilivyoidhinishwa na TCRA.
6. Kutokuchakachua simu au laini ya simu. Hii inahusu hasa mafundi wa simu na wamiliki wa simu husika. Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, kifungu cha 129 kimeweka adhabu dhidi ya kuchakachua simu au laini na kifungu 135 kimeweka adhabu dhidi ya kufungulia simu ambayo imefungiwa kama sehemu ya kutekeleza mpango wa rajisi kuu ya
namba tambulishi.
7. Ukipokea simu kwa ajili ya matengenezo au kwa huduma ya kuchaji, hakikisha aliyekupa ana uthibitisho wa umilki wa simu hiyo au kifaa hicho na pale inapowezekana aonyeshe risiti ya manunuzi ya kifaa husika. Weka, tumia na tunza kitabu cha kumbukumbu (rejesta) ya vifaa vyote
vinavyopokelewa na kutoka. Vilevile hakikisha kuwa wahusika wanaweka sahihi zao.
Faida za kutumia Mfumo wa anwani mpya za kitaifa na postikodi