Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayecheza club ya Paris Staint Germain ya Ufaransa Angel Di Maria amefunguka na kueleza ukweli tofauti yake na kocha wake wa zamani wa Man United Louis van Gaal ambaye alipelekea Di Maria kuihama Man United na kwenda PSG.
Angel Di Maria alihama Man United na kwenda PSG akiwa kadumu na club hiyo kwa msimu mmoja (2014-2015) na baadae kujiunga na PSG wakati huo ikifundishwa na kocha wa Arsenal wa sasa Unai Emery ambaye Di Maria anakiri kuwa alichangia kumrudisha katika hali ya kujiamini zaidi.
“Nilikuwa Man United na kila kitu kilikuwa sawa na Louis van Gaal miezi miwili ya mwanzo, baada ya ugomvi mmoja mambo hayakuwa tena sawa kila kitu hakikuwa kama mwanzo, ugomvi kati yangu na Van Gaal ulitokea kwa sababu alikuwa akinionesha vitu vibaya na hasi ambavyo vilikuwa vinanirudisha nyuma” >>> Di Maria
“Siku moja tuligombana nikamwambia kitu kimoja sitaki kuona hivyo vitu vikijirudia tena, hapo nilikuwa nikifanya vitu kwa uzuri na kumuuliza kwa nini hanioneshi vitu vizuri, hakupenda namna nilivyokuwa naongea nae, kuanzia hapo ndio matatizo yalipoanzia”>>>Di Maria
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba