Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 bora katika ligi ya Europa alhamisi iliyopita, Arsenal watakuwa jijini London katika uwanja wao wa nyumbani, Emirates Stadium kukabiliana na BATE Borisov katika mechi ya marudiano ya kufuzu hatua ya 16 Bora Alhamisi hii.
Arsenal walipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa goli moja na BATE ya nchini Belarus, katika mchezo huo mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette alionyeshwa nyekundu dakika ya 85 hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza jijini London usiku wa Alhamisi.
Nafuu kwa kocha Unai Emery ni kurejea kwa mshambuliaji Pierre Emerick Aubameyang ambaye aliukosa mchezo wa kwanza kwa ugonjwa. Pengine alhamisi tutamshuhudia Mesut Ozil akipewa nafasi ya kucheza baada ya mashabiki wengi wa klabu hiyo kulalamikia Ozil kuachwa nje ya kikosi licha ya kuwa yuko fiti kucheza.
Kwa upande wa Chelsea wao wanatarajia kufuzu kufuatia ushindi wa magoli 2-1 walioupata ugenini dhidi ya Malmo FF Alhamisi ya wiki iliyopita katika mchezo wa kwanza. Licha ya kupoteza dhidi ya Manchester United siku ya Jumatatu Chelsea watatarajia kupumzisha baadhi ya wachezaji ili kuwaweka fiti kwa ajili ya mechi ya fainali ya Kombe la ligi, Uingereza siku ya Jumapili, Europa League inaoneshwa na Star Times pekee.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba