Club ya Chelsea ya England kwa sasa zinasambaa tetesi kuwa inawezekana ikafanya maamuzi magumu kwa mara nyingine tena na kuamua kumfuta kazi, kocha wao mkuu Maurizio Sarri akiwa ndio kwanza anaelekea kumaliza mwaka mmoja toka ajiunge na timu hiyo akitokea Napoli ya Italia.
Toka club ya Chelsea iwe chini ya Bilionea Roman Abromovich imefuta kazi jumla ya makocha tisa na kama itaamua kumfuta kazi Maurizio Sarri basi itakuwa inaingia hasara ya pound milioni 5 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 15 kama fidia, hadi sasa Chelsea tokea mwaka 2004 imelipa jumla ya pound milioni 89.3 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 269 kama fidia ya kuvunja mikataba ya makocha.
Kwa sasa club ya Chelsea inahusishwa kwa karibu kuhitaji huduma ya makocha wawili, pamoja na kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane ambaye yupo radhi kujiunao kama watamuongezea mkataba Hazard na kumpa pound milioni 200 afanye usajili.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba