Tunayo story kutokea kwa Wananchi wa Mji Mwema Kigamboni ambapo wamehoji kuhusu Mpango Kabambe wa Jiji la Dar es Salaam 2016\2036 unaoweka mikakati ya maendeleo ya jiji na maeneo yanayolizunguka.
Wananchi hao wamewahoji watalaamu wanaosimamia mpango huo kwamba ni vipi wanaweza kunufaika, lakini pia wanahisi kama wanaongopewa kwa sababu walishapata hasara ya kuzuiwa kujengwa kwa madai ya uwepo wa mpango kama huo.
Akijibu baadhi ya hoja, Mtalaamu na Mshauri wa mpango huo, Camillius Lekule amesema kuwa hata yeye alishawahi kusema kwamba Mji Mpya wa Kigamboni hauwezekani na aliambiwa atafungwa.