Msanii wa filamu Wema Sepetu amekana kuchapisha video za ngono kupitia ukurasa wake wa Instagram katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo kesi yake inatarajiwa kuanza kusikilizwa Machi 18, 2019.
Hatua hiyo inatokana na msanii huyo kusomewa maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde na Wakili wa serikali, Glory Mwendi ambaye alianza kwa kumkubushia shitaka Wema.
Wakili Mwendi ameeleza kuwa mshitakiwa anaitwa Wema Izac Sepetu(30), anamiliki akaunti ya Instagram ya Wema Sepetu na alirekodi video ya Ngono October 18,2018.
Hakimu Kasonde alimtaka Wakili Mwendi kueleza ama kudadavua hiyo video ya ngono ikoje ama ni kitendo gani kilichofanywa na Wema, ambapo alijibu kuwa video inamuonyesha Wema akinyonyana ndimi na mwanaume.
Ameeleza kuwa October 25, 2018 Maafisa wa TCRA waliiona video hiyo na kuiripoti kituo cha Polisi Kijitonyama.
Baada ya kuripotiwa upelelezi ulianza na October 29, 2018 alikamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi ambapo alihojiwa na kukana maelezo hayo kisha kufikishwa mahakamani November 1, 2018.
Katika maelezo hayo,Wema alikubari wasifu wake ikiwemo majina, anuani na umriwake huku akikana kurekodi na kuchapisha video hizo katika akaunti yake.Pia alikiri kukamatwa na kupelekwa Polisi.Hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi March 18, 2019 kwa ajili ya kusikilizwa.