Moja kati ya habari kubwa iliyotawala wakati wa kukaribia kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, namna ambavyo waliingia na mavazi ya kipekee ya asili ya taifa lao la Nigeria, hiyo ikiwa ni tofauti na mataifa mengi sana yalioshiriki michuano hiyo waliwasili Urusi wakiwa wamevaa suti.
Mavazi ya Nigeria yalikuwa gumzo na mvuto ambao ulipelekea hata jezi zao kusifiwa kuwa ni nzuri zaidi, inadaiwa kuwa inakaribia mwaka mmoja sasa lakini shirikisho la soka Nigeria NFF, wanadaiwa pesa na mbunifu wa mavazi hayo aliyowavalisha wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria.
Mbunifu wa mavazi hayo aliyowavalisha wachezaji wa Nigeria Esimaje Awani, ameendelea kulalamika katika mitandao ya kijamii kuwa bado hajalipwa pesa za kufanya kazi hiyo, baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakimshauri kuwa aende Mahakamani.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake