Kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp ametoa kauli hadharani inayoashiria kuonekana kumuunga mkono kocha wa muda wa Man United Ole Gunnar Solskjaer kuwa apewe timu hiyo jumla, baada ya Man United kumtangaza Ole Gunnar Solskjaer na kumfuta kazi kocha wao wa kudumu Jose Mourinho kwa madai ya mwenendo mbaya wa timu yao.
Man United walitangaza kuwa Ole Gunnar Solskjaer anakalia kiti cha ukocha wa Man United kwa muda tu hadi mwisho wa msimu lakini kutokana na kufanya baadhi ya mabadiliko ya nje na ndani ya uwanja na timu kuanza kupata matokeo chanya, kocha wa Liverpool anaamini kuwa Solskjaer atapewa timu hiyo jumla kutokana na kurudisha taratibu za Sir Alex Ferguson za zamani katika timu hiyo.
Kuelekea game dhidi yao siku ya Jumapili Klopp anaamini Solskjaer atapewa kazi ya kudumu“Hakuna shaka ana ubora na anastahili kupewa kazi jumla kwa asilimia 100 kwa sasa yeye ndio kocha na hakuna mashaka ataendelea kuwa kocha (Man United) mwaka ujao tena hilo liko wazi”
Jurgen Klopp akiwa na Liverpool ndio anakutana na Man United kwa mara ya kwanza ikiwa na kocha wao mpya wa muda Ole Gunnar Solskjaer, Solskjaer toka amejiunga na Man United ameshinda michezo 11 kati ya 13 na akipoteza mchezo mmoja pekee wa UEFA Champions League 16 bora msimu huu dhidi ya Paris Saint Germain.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake