Moja kati ya matukio makubwa yaliojitokea katika mchezo wa fainali ya michuano ya EFL kati ya Chelsea dhidi ya Man City, ni kitendo cha golikipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga kukataa kufanyiwa mabadiliko wakati wa mchezo huo ili aingie mwenzake Caballero kitu ambacho kilikuwa gumzo mitandaoni.
Kocha Maurizio Sarri aliamua kufanya mabadiliko dakika ya 119 ili aingiea golikipa Caballero ambaye kimsingi alikuwa anamuingiza kwa ajili ya kucheza mikwaju ya penati kwani ndio hatua iliyokuwa inafuata, baada ya dakika ya 120 kuelekea kumalizika 0-0 lakini Kepa aligoma kufanyiwa mabadiliko ndipo Caballero ilipomlazimu arudi kukaa.
Hata hivyo licha ya Kepa kugoma kufanyiwa mabadiliko hayo na kutaka mikwaju ya penati kucheza mwenyewe, Chelsea iliishia kupoteza game hiyo kwa kufungwa kwa mikwaju ya penati 4-3, hivyo game ikamalizika kwa Kombe hilo kuelekea katikati ya jiji la Manchester ambako ndio Makao makuu ya Man City.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake