Kwa timu zilizosalia kwenye Coppa Italia, michuano hiyo ndio nafasi ya wazi au nafasi pekee kwa timu hizo kushinda Kombe msimu huu, baada ya kutolewa kwa Juventus ambao wameshinda kombe hilo kwa miaka minne mfululizo timu za AC Milan, Fiorentina, Lazio na Atalanta iliyowafunga Juventus katika robo fainali watategemea kushinda Kombe hilo.
Bahati nzuri hatua ya nusu fainali huwa na mechi za marudiano. Hii inatoa fursa kwa timu zote kutumia vizuri viwanja vya nyumbani, Lazio dhidi ya AC Milan ndiyo mechi ya kwanza, mchezo huo utapigwa katika dimba la Stadio Olimpico, Lazio ambao ni maarufu kama I Biancocelesti, wao wanatafuta kushinda Kombe la Coppa Italia kwa mara ya saba, watapambana dhidi ya wenzao wa jiji la Milan.
Kwa upande wa AC Milan watategemea magoli kutoka kwa mshambuliaji wao mpya Krzysztof Piatek aliyejiunga nao akitokea Genoa baada ya Gonzalo Higuain kujiunga na Chelsea, mshambuliaji huyo raia wa Poland amekuwa katika kiwango kizuri tangu ajiunge na AC Milan, amefunga magoli saba katika mechi sita, huku magoli yake mawili yakiwaondoa Napoli katika michuano hiyo.
Mchezo wa Lazio vs AC Milan utapigwa Jumanne saa 5:00 huku siku ya Jumatano Fiorentina watacheza dhidi ya Atalanta, licha ya kuwahi kufika fainali mara tatu pekee, timu ya Atalanta wanaamini wana kila sababu ya kushinda Kombe hasa baada ya kuwang’oa mabingwa Juventus kwa ushindi wa kuvutia 3-0 mashabiki wao wana kila sababu ya kuamini huu ni mwaka wao na zitaoneshwa na Star Times.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake