Masuala ya watumiaji yamewekwa bayana kwenye sheria mama na kanuni mbalimbali ambazo ni:
1. Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya 2003. Sheria hii imefafanua majukumu na kazi za TCRA kuhusiana na watumiaji. Aidha kifungu cha 20 kimeweka utaratibu wa kuanzisha Kamati ya Malalamiko na kifungu 40 kinaweka utaratibu wa kuwasilisha malalamiko na kifungu kidogo cha saba (7) kinaelezea kuwepo, ndani ya TCRA, kwa kitengo maalum cha kushughulikia malalamiko.
2. Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA). Sheria hii inaelezea haki na
wajibu wa watumiaji katika masuala mbalimbali kuhusiana na umilki na matumizi ya vifaa na huduma za mawasiliano. Aidha kifungu cha 98 na 99 kimeweka utaratibu wa kulinda faragha za watumiaji.
3. Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015 ina vifungu 59 ambavyo kati yake vifungu 19 vya sheria hiyo vinahusu namna ambavyo mtumiaji analindwa.
4.Kanuni za EPOCA za kumlinda mtumiaji.
5.Kanuni za Maudhui.
6.Kanuni za EPOCA za Leseni.
7.Kanuni za EPOCA za Ubora wa huduma.
8.Kanuni za EPOCA za Huduma za ziada.
9 Kanuni ndogo za kusimamia matumizi ya huduma na bidhaa za mawasiliano
kwa watumiaji wenye ulema