Kitengo hiki ni timu yenye jukumu la kitaifa katika kuratibu matukio ya usalama katika mitandao na pia kushirikiana na vyombo vingine vya kikanda na kimataifa katika kusimamia matukio ya usalama mitandaoni. TZ-CERT inatoa huduma zifuatazo:
1. Kushughulikia matukio ya kiusalama yaliyotokea na kuzuia madhara zaidi.
2. Uchambuzi wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali.
3. Kutoa taarifa kwa umma na wadau kwa maeneo ambayo yameonekana kuwa na udhaifu.