Kesi ya kutoa maneno ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe imekwama kuanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu shahidi amepata udhuru.
Hayo yameeelezwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kusikilizwa. Hata hivyo, Wakili Wankyo ameeleza kuwa shahidi waliyepanga kuwa naye amepata udhuru, hivyo wanaomba ahirisho la muda mfupi.
MSIBA WA RUGE: MSTAAFU KIKWETE “NIMELEMEWA, HUZUNI, MAJONZI, TAIFA LIMEPOTEZA MTU MAHIRI