Moja kati ya habari zinazozungumzwa sana baada ya kubainika kuwa ndege ndogo iliyokuwa imembeba marehemu Emiliano Sala ambaye ni mshambuliaji mpya wa Cardiff City, kuwa haikuwa imesajiliwa kubeba abiria, hivyo kabla ya Cardiff kulipa hela za usajili wa mchezaji huyo walitaka kujua kama alitafutiwa usafiri na nani.
Awali wakala wa mchezaji huyo Willy McKay alituhumu kuwa Cardiff City ilimtelekeza hotelini Emiliano Sala baada ya kusaini mkataba wao wa miaka mitatu akitokea Nantes FC kwa dau la pound milioni 15, kitu ambacho kinadai kuwa ni uongo kiasi cha Cardiff kuvujisha meseji zao za mwisho kuwasiliana na Emiliano Sala kuhusiana na kumtafutia ndege ila alikataa baada ya kujazwa maneno na wakala wake.
“Alitelekezwa hotelini hadi akafikia hatua ya kuandaa usafiri mwenyewe, hakuna mtu yoyote Cardiff alikuwa akionekana anafanya chochote kwa ajili yake (Sala), wamemnunua mchezaji kwa pauni milioni 15 halafu wanamtelekeza hotelini anaanza kuangahika mwenyewe kutafuta ndege ”>>>Willy McKay
Bado kunadaiwa kuwepo na mvutano kabla ya Cardiff City kukubali kulipa pound milioni 15 kwa Nantes FC kama ada za usajili, kwani mchezaji huyo wanadai mauti yalimfika January 21 2019 siku tatu baada ya kusaini, Cardiff hivyo wanatafuta njia za kukwepa kulipa ada hiyo.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake