Mtanzania Ally Ng’anzi ambaye alikuwa zao la timu ya taifa ya vijana ya Tanzania wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys walioshiriki michuano ya AFCON U-17 nchini Gabon, nyota yake inaendelea kung’aa baada ya kufanikiwa kupata timu mpya.
Ally Ng’anzi ambaye pia amecheza timu ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 20, miezi michache iliyopita alipata nafasi ya kujiunga na club ya MFK Vyskov ya Jamhuri ya Czech akitokea Singida United ya Tanzania.
Baada ya kudumu na MFK Vyskov kwa miezi michache tu Ally Ng’anzi ametolewa kwa mkopo wa mwaka mmoja kwenda kucheza katika club ya Minnesota United FC ya nchini Marekani inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS) hiyo ni fursa kubwa kwa Ally Ng’anzi katika maisha yake ya soka.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake