Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezitaka Halmashauri kuhakikisha zinashirikiana vizuri na Walimu kuhakikisha wanainua kiwango cha elimu katika Shule za Sekondari hususani kwa watoto wa kike ambao wameonekana matoeo yao sio mazuri.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Ndalichako wakati wa ziara yake Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma ambapo amesema Serikali inatumia zaidi bilioni 24 kwa ajili ya elimu bure pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya elimu hivyo ni lazima kuhakikisha nguvu za Serikali hazipotei bure kwa wanafunzi wengi kufanya vibaya katika mitihani yao.