Tanzania inatekeleza huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani, ambapo mtumiaji anabaki na namba yake ya awali iwapo ataamua kuhamia
mtandao mwingine wa simu za kiganjani nchini.
Nani anaweza kutumia mfumo huu? Huduma hii itatumiwa na wateja Tanzania wanaolipia huduma kwanza na wanaolipia huduma baada ya matumizi. Ili kuingia kwenye mfumo huu, laini ya simu ya mtumiaji lazima iwe inatumika, yaani haijafungiwa au kusimamishwa kwa muda.
Itagharimu kiasi gani kuhama na namba? Hakuna gharama za kuhama na namba. Hata hivyo, kabla ya kuhama itabidi mtumiaji anunue laini mpya ya simu za kiganjani kutoka kwa mtoa huduma mpya.