Ikiwa ni Siku ya Wanawake Duniani tunayo stori kutokea kwa Serikali ya Marekani kupitia Kaimu Balozi wake nchini Tanzania Dk.Inmi Patterson ambapo amezungumza na Wasichana wanaojihusisha na masuala ya Teknolojia kupitia Taasisi ya Apps&Girls.
Dk.Patterson amesema wasichana wengi wanaacha shule wakati wa kubalehe na kuolewa ama kudharauliwa na kulazimika kutoudhuria shuleni kwa sababu ya hedhi, hivyo lazima kuwekezwa kwa wanawake na wasichana kwani ndio ufunguo wa kizazi kijacho.
“Wanawake wanapendelea kuwekeza zaidi mapato yao kwa ajili ya familia zao ikiwa ni mara 10 kuliko wanaume, ambapo Tanzania ina chini ya asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa miaka 20 hadi 24 waliomaliza elimu ya Sekondari,“amesema.