Serikali ya China imesitisha matumizi yote na usafiri wote wa ndege sawa na ile ya Ethiopia Airlines Boeing 737 Max 8 siku moja baada ya Boeing 737 Max 8 mali ya shirika la Ethiopian Airlines iliyoanguka jana na kuua watu 157 ikiwa katika safari zake kutoka Addis Ababa kwenda Nairobi pamoja na Indonesian Airlines (The Lion).
Hadi Januari 2019, China ilijumuisha 20% ya Boeing 737 Max zinazotumika duniani, hivyo hatua hiyo inaweza kuathiri soko la ndege hizo.
Nayo kampuni ya Boeing ambayo ndiye mtengenezaji wa ndege za Boeing 737 Max 8 imelazimika kusitisha mpango wa kuzindua ndege yake mpya aina ya Boeing 777X, iliyokuwa inatarajiwa kuzinduliwa Machi 13, 2019, kufuatia ajali ya Boeing 737 Max 8.
Ndege hiyo ya kisasa (Boeing 777X) ina uwezo wa kubeba abiria 425 na zitaanza kutumika mwaka ujao.
MCHUNGAJI MGOGO KATIKA UBORA WAKE “PASUA KICHWA NI MMEO, UNAWEKA MISUMARI NA BOKO HARAMU”