Kutana na Kijana Anganile Mwambuluma(45), Mkazi wa Kijiji cha Mshikamano Mbalizi, Mbeya Vijijini ambaye ni mpiga debe stendi ya daladala Mbalizi huku akimiliki Shule ya Sekondari.
Anasema hakuna mtoto wake anaesoma inayomilikiwa na Serikali kutokana na kile anachodai kuwadhibiti na utoro wa kutohudhuria vema masomo kama uliomkuta yeye, hapendi ujitokeze kwa watoto wake.
Anganile alizaliwa Agosti 17, 1973, katika Kijiji cha Mapinduzi, Kata ya Utengule Usongwe, Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya na ni mtoto wa 10 kwa Baba yake mzazi, lakini ni mtoto wa nne katika uzao wa tumbo la mama yake mzazi.
“Miaka ya 1994, nikaungana na marehemu Safari, ambaye alikuwa na gari aina ya Hiace, nikawa kondakta wake, tukaenda kuchemka na kufanya safari za Mpemba Wilaya ya Mbozi na Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya, ndipo niliokota kwenye gari Tsh. 60,000/= nikachanganya na niliyokuwa nayo Tsh.80,000/= nikarudi nyumbani na kufungua kiosk” Anganile