Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametangaza utaratibu ambao atakuwa anautumia yeye pamoja na Watendaji wengine wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wa kusafiri kwa kutumia daladala pale wanapotakiwa kuongozana kwa pamoja kwenda kukagua baadhi ya maeneo.
Akizungumza ndani ya daladala Chalamila amesema wameamua kutumia usafiri huo badala ya kutumia magari ya Serikali ili kupunguza gharama za mafuta.
“Tunalipa nauli kama abiria wengine na huu usafiri ni mzuri maana unatusaidia kupunguza gharama za mafuta, tutaendelea kuutumia,” Chalamila.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Mbeya James Kasusura alisema utaratibu huo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuwataka Viongozi wa umma kuacha tabia ya kuwa Miungu watu.
JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YALENGA KUWANUFAISHA WANAOZUNGUKA ZIWA VICTORIA