Rais John Magufuli ametoa Bilioni 3 katika mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mbili katika wilaya za mkoa huo ambapo hospitali moja inatarajiwa kuwa na wahudumu 250 kwa ajili ya kuongeza huduma za afya.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambapo amesema fedha hizo zimeshaingizwa katika mifuko ya Halmashauri ya Ilala na Kigamboni ambapo ujenzi wa hospitali hizo unatakiwa uwe wa kasi ili ifikapo Juni 31, 2019 ziwe zimekamilika.
“Mmepata Rais anayependa afya za watu ziimarike, ambapo katika mkoa wetu tumepata pesa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali za wilaya mbili lengo ni kuhakikisha wananchi wa Dar es Salaam wanazidi kupata afya bora kwa maana haupaswi kusafiri umbali mrefu kufata hospitali ambapo hospitali moja itakuwa na waudumu 250,“amesema.