Zipo haki ambazo zimewekwa kwenye sheria; nazo ni usalama wa huduma zinazotolewa, usiri
na faragha wakati wa matumizi na elimu kuhusu huduma zinazotolewa.
Haki hizo ni: Usalama na Ulinzi: Watumiaji wanatarajia kutumia huduma na bidhaa ambazo ni salama na imara. Mtoa huduma, muagizaji au msambazaji wa vifaa vya mawasiliano hapa nchini, anapaswa kuhakikisha kwamba vifaa vyake vyote vinakidhi mahitaji ya usalama wa afya kabla ya kutumiwa na wateja.
Vifaa vya mawasiliano vinavyoingizwa Tanzania vinatakiwa kuthibitishwa ubora wake na TCRA,
kuwa salama kwa watumiaji kwa kuzingatia viwango vya ubora wa kimataifa.
Kuwa na usiri au faragha katika matumizi: Sheria inamlinda mtumiaji dhidi ya kutolewa kwa taarifa zake na mtoa huduma kwa watu wasiohusika. Watumiaji wana haki ya usiri au faragha katika matumizi ya huduma.
Sheria imeweka masharti ya uaminifu kwa watoa huduma ili kuhakikisha na kudumisha usiri wa maudhui ya mawasiliano yote, ziwe data au taarifa zozote ambazo mtoa huduma anaweza kuvipata kutokana na kumhudumia mteja.
Taarifa za mteja hazitatolewa kwa mtu yeyote bila ya ridhaa ya maandishi ya mteja mwenyewe. Taarifa zinaweza kutolewa kwa wahusika walioidhinishwa pale tu ambapo zinahitajika katika uchunguzi wa matukio ya kijinai na kwa utaratibu uliowekwa kisheria na kikanuni au itakapoombwa na mahakama.
Elimu kwa Watumiaji: Watumiaji wana haki ya kuelimishwa kuhusu huduma wanazotarajia
kujiunga nazo na zile zinazotolewa kwao na masuala yanayohusiana na matumizi yao