Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata watu wawili ambao ni Ladislaus Peter Mkimu na William Ngalivuva wote wakazi wa Jiji la Arusha kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi (ACP) Jonathan Shana, alisema kwamba tukio hilo lilitokea muda wa saa 4:00 Asubuhi katika eneo la Mjini Kati jirani na hospitali ya Saint Thomas.
“Mara baada ya kupata taarifa toka kwa msiri, askari wetu walianza kufuatilia na walipogundua waliweka mtego uliofanikisha kuwakamata watuhumiwa hao, ambao awali walikutwa na kiasi kidogo cha noti hizo na katika mahojiano watuhumiwa hao walikiri kuwa na noti nyingine kwenye makazi yao eneo la Lemara ambapo zilipatikana noti 1,697’’ Kamanda Shana.
“Jumla ya noti hizo bandia zilizopatikana ni Dola 16,200 zenye thamani ya fedha za kitanzania Shilingi 37,260,000 na zingeweza kuleta athari kubwa katika uchumi wa nchi yetu”. aliongeza Kamanda Shana.
UFA KATIKA GHOROFA LA NHC MBEYA, MENEJA AMETOA RIPOTI BAADA YA TETEMEKO KULIPITIA