Baada ya nahodha wa Taifa Stars kutumia ukurasa wake wa instagram kuandika na kuomba kuwa TFF wasimsahau Shomari Kapombe katika mgao wa zawadi wa wachezaji waliyoipeleka Taifa Stars fainali za AFCON 2019 Misri, imeonekana ombi lake limefanyiwa kazi na kuipongeza TFF kuwa haijawasahau wachezaji wote waliohusika kuipambania nchi toka mwanzoni.
Samatta kupitia twitter account yake alifuta tweet yake ya mwanzo na kuipongeza TFF kuwa na mpango wa kuwazawadia wachezaji wote, Rais Magufuli alitoa kiwanja kwa kila mchezaji na RC Paul Makonda alitoa Tsh milioni 10 kwa kila mchezaji aliyefanikisha timu kufika AFCON kupitia kamati yake ya uhamasishaji.
“Tuwapongeze shirikisho mpira wa miguu Tanzania kwani linamipango na wachezaji wote walioshiriki katika kampeni hii ya kuwania tiketi na kwa heshima yao basi naondoa Twitte yangu iliyopita kwani tayari mipango ipo barabara kwa kila mchezaji aliyeshiriki. asanteni TFF”>>>Samatta
ama utakuwa unakumbuka vizuri Shomari Kapombe aliumia mwishoni mwa mwaka jana akiwa na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars katika mazoezi ya mwisho Afrika Kusini kuelekea Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza AFCON 2019, toka ameumia Kapombe hajarudi uwanjani rasmi hadi Taifa Stars inacheza na Uganda.
MUHIMBILI JKCI NAO WATANGAZA NUSU BEI KWA USHINDI WA TAIFA STARS