Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa ufafanuzi wa namna ya uuzaji tiketi katika Viwanja vya soka katika mashindano mbalimbali ya mechi za Mikoani na jijini Dar es Salaam.
.
Katika tiketi zote ambazo zinakatwa katika michezo ya Mikoani zinasimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kwa Viwanja vya Dar es Salaam, zoezi hilo linasimamiwa na wamiliki wa Viwanja.
.
TFF katika zoezi hilo imekuwa ikitaja bei ya tiketi na madaraja yake na kuacha kazi kwa mamlaka husika za TAMISEMI na Uwanja kupanga namna ya ukusanyaji wa mapato kupitia tiketi, hivyo TFF haina dhamana ya kuuza tiketi.
.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Uganda Jumapili ya March 24 2019 ilidaiwa kuwa ziliuzwa tiketi zaidi ya uwezo wa uwanja na hata Rais Magufuli wakati anaongea na wachezaji wa Taifa Stars aligusia suala hilo.
.
MUHIMBILI JKCI NAO WATANGAZA NUSU BEI KWA USHINDI WA TAIFA STARS