Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametembelea hanga la matengenezo ya ndege la Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini DSM na kukagua marekebisho ya ndege ya Serikali aina ya Foker 50 ambayo inabadilishwa matumizi ili itumike kusafirisha abiria kama zinavyotumika ndege nyingine za ATCL.
Katika ziara hiyo ya kushtukiza Rais Magufuli ameshuhudia kazi ya ufungaji wa viti 48 vya abiria ukiwa umekamilika na mafundi wa kupaka rangi wakiwa wanakamilisha kuchora picha ya mnyama Twiga anayetumiwa kama nembo ya ndege za ATCL.
Rais Magufuli ameelezwa kuwa kazi ya marekebisho ya ndege hiyo imechukua muda wa siku 7 na mafundi wanakabidhi ndege leo, tayari kwa matumizi.
Hata hivyo mapema leo asubuhi akipokea taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha viongozi na watendaji wa Serikali kutaka kupeleka ndege (Foker 50) Afrika Kusini ili ikabadilishwe rangi ambako ingetumia gharama kubwa ya kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 328 badala ya kazi hiyo kufanyika hapa hapa nchini.
SIKU YA NNE MWILI UMETOLEWA CHINI MAWE, DC APIGA MARUFUKU MGODI KUFANYA KAZI