Club ya Leicester City Jumamosi hii ya March 30 2019 itasherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya mmiliki wa club hiyo marehemu Vichai Srivaddhanaprabha, uongozi wa Leicester City ili kumkumbuka na kumuenzi Mr Vichai Srivaddhanaprabha wamepanga kuwa Jumamosi hii itakuwa siku maalum.
Leicester City Jumamosi hii itakuwa katika uwanja wao wa King Power kucheza dhidi ya AFC Bournemouth, hivyo ili kusherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya marehemu Mr Vichai Srivaddhanaprabha kila shabiki atakayekuwa anaingia uwanjani atapewa bia au maji na cupcake.
Mmiliki na mwenyekiti wa timu hiyo Vichai Srivaddhanaprabha alifariki October 29 2018 akiwa katika helicopter yake binafsi iliyoanguka dakika chache baada ya kupaa kutokea uwanja wa King Power, alipokuwa anaangalia game ya Leicester City dhidi ya West Ham United iliyomalizika kwa sare ya 1-1.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars