Moja kati ya watu ambao huwa hawajiweki sana na ushabiki wa wa soka wa moja kwa moja ni viongozi wa dini, haijajulikana kwa nini lakini ni nadra kusikia viongozi wa dini wakitoa maoni kuhusu mchezo wa mpira wa miguu au hata kuweka wazi hisia zao katika mchezo huo.
Kauli kubwa iliyoshitua wengi ni kuhusiana na kauli ya kiongozi wa dini ya kikatoliki Pope Francis akiongea na La Sexta TV “Bila shaka ni furaha kumuona Lionel Messi akicheza lakini sio Mungu” kauli hiyo ameitoa kuhusiana na baadhi ya mashabiki kupenda kumuita Messi kama Mungu wa mpira.
Lionel Messi ni miongoni mwa wachezaji wachache hapa duniani ambao wameweza kucheza kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu zaidi, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wameweka rekodi ya kipekee katika tuzo ya Ballon d’Or kila mmoja akitwa mara tano, hii ni rekodi inayoaminika kuwa itadumu kwa muda mrefu.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars