Kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Congo DRC na club ya TP Mazembe Robert Kidiaba amewasili Tanzania akiwa na kikosi cha timu ya TP Mazembe kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya CAF Champions League dhidi ya Simba SC siku ya Jumamosi.
Kidiaba kwa sasa ni mbunge wa jimbo la mkoa wa Katanga baada ya kuchaguliwa hiyo ni baada ya kustaafu kucheza soka lakini pia ni kocha wa makipa wa TP Mazembe wa sasa, baada ya kutua Tanzania na kuulizwa ishu za Ubunge ameweka wazi kuwa ameamua kuwatumikia mahali alipotoka.
“Najua kama kuja kwa Bunge ni Mungu ndio alinipatia ile cheo, najua kwetu siwezi kusahaulika hata mara moja kule ninapotokea nipo kwa Bunge Mungu apewe sifa, kule mimi nimetokea kwa mpira kwa hiyo sitaki kusahaulika Mungu apewe sifa”>>> Robert Kidiaba
Kwa sasa Robert Kidiaba ana umri wa miaka 43 na ameamua rasmi kuwa kocha wa magolikipa wa TP Mazembe aliyoichezea kwa muda wa miaka 14 toka alipoamua kujiunga na timu hiyo 2002 akitokea AS Saint Luc, Kidiaba alistaafu kucheza soka 2016 na alikuwa kipa wa timu ya taifa ya Congo.
Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….