Bibi Patilo Kamote mkazi wa Wilaya ya Lushoto Tanga amesema wakati akiwa kwenye basi kuelekea Nzega Mkoani Tabora alikerwa na kondakta baada ya kugoma kumpa ashike begi lake ambalo lilikuwa na ‘uganga wake‘ nakusema alikwazika na baada ya kupelekwa maeneo ya stendi ya Arusha alianza shughuli zake za ‘uganga’ nakubaini alikuwa amekwazwa.
“Walinishusha kwenye gari bila kuniambia sababu, mwishoe wakaja Askari kunihoji, baada ya hapao walinirudishia nauli, wakanitafutia bodaboda wakanipeleka Polisi kwa ajili ya usalama, wao walijua Mimi ni mganga” Bibi Kamote