Leo April 4, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akiwa Mtwara amesema “Unakuwa una tatizo fulani unakimbilia kuchoma Ambulance, walioshiriki kuchoma Ambulance walaaniwe, mtafika siku moja mtachoma Kituo cha Afya, Serikali inaweka hela nyie mnachoma, hasira za namna hiyo kama ni pepo mkakemee”
“Sasa Mbunge anahangaika na si ajabu waliochoma ndo wanasema hatuna Ambulance, sababu ni Mbunge hawezi sema mliochoma, Mimi nasema mliichoma na hamkutakiwa kupewa hata bajaji, ili mjifunze” Rais Magufuli
“Waliofanya kitendo hiki ni watu wachache saivi wakina Mama, Wazee wanateseka, tunaambiwa tusamehe, Mbunge nitakupa Ambulance nyingine mpya” Rais Magufuli
“Ole wenu mlichoma sijawa Rais tungetafutana tu, Ambulance imechomewa hapa unashika Kijiji chote, watakula push-up, watalamba michanga watasemana tu” Rais Magufuli
RC MAKONDA “WATU WA HOVYO WANAONEKANA WA MAANA, MTANDAONI HAPAKO SALAMA”