Shahidi wa nane Samweli Tesha kwenye kesi ya mauaji ya Mwanafunzi wa Shule ya Scolastica amesema alipigiwa simu na Bwana Afya wa Manispaa kuchukua mwili na kwenda kuzika ambapo aliambatana na kondakta na dereva kuzika katika makaburi ya Karanga.
Kesi hiyo imeendelea leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi mbele ya Jaji Filmin Matogolo ambapo mashahidi wameendelea kutoa ushahidi.
Ameendelea kwa kusema kuwa mwili waliouzika ulikuwa umeharibika na unakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 16-17 na alikuwa amevalia bukta, soksi huku kanga ikiwa imefunika kwa juu na baada ya kuzika alichomeka mti miguuni pale inapotokea mtu hafahamiki ili baadae kama atajitokeza mtu iwe rahisi kufukua.