Kocha wa kireno aliyewahi kuvifundisha vilabu vya Porto, Chelsea, na Tottenham Andre Villas-Boas amethibtishwa kuwa kocha wa Zenit St Petersburg akimrithi kocha Luciano Spalletti.
Kocha wa kiitaliano Spalletti alitimuliwa na klabu hiyo ya Russia wiki iliyopita baada ya kukaa kwenye timu hiyo kwa miaka mitano kufuatia mwenendo mbaya wa timu katika ligi na ulaya, baada ya kuchapwa 4-2 na Borrusia Dortmund katika mchezo wa kwanza raundi ya 16 bora.
Na Villas-Boas, ambaye amekuwa hana kazi tangu alipofukuzwa na Tottenham mwezi December mwaka jana amechukua nafasi yake kwa kusaini miaka miwili.
“Zenit wamefikia makubaliano ya mkataba wa miaka miwili na kocha Andre Villas-Boas,” taarifa ya klabu ilisema.
“Mkataba utasainiwa na Villas-Boas atatambulishwa mjini St Petersburg kuwa kocha mkuu mpya wa Zenit March 20. Mkataba wa Villas-Boas unaanza March 2014 na utaendelea kwa miaka miwili.”