Wakati mijadala ikiendelea kuhusu Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini (CAG), Prof Mussa Assad, CAG Mstaafu Ludovick Utouh amesema kuwa CAG ndio jicho la wananchi kwa kuwa wao ndio wenye mali na rasilimali za nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa Wanawake Viongozi nchini uliowahusisha Wahasibu, Utouh amesema ripoti ya CAG inaenda bungeni kwa sababu ndio wawakilishi wa watu.
“CAG anapokagua na kuleta mapendekezo, mapendekezo yale yanalenga katika kuboresha utendaji wa aliyemkagua iwe taasisi ama serikali na inapokuwa anakagua na hakuna dhamira ya kutekeleza mapendekezo yake kwa dhati inaathiri dhana ya utawala bora na uwajibikaji katika nchi,“amesema.