Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizoelekezwa kwa Rais wa TFF kupewa fedha na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) zinazodaiwa ni fedha za rushwa, Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred amefafanua kwa kina tuhuma hizo.
.
Kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF iliyokutana Mei 8,2017 Bahrain kilipitisha maamuzi ya fedha mbalimbali uliokua na mchanganuo wa sehemu ya maendeleo na kiasi kingine kikielekezwa kwa Marais wa Mashirikisho Barani Afrika kuwasaidia katik mizunguko mbalimbali ya mpira wa miguu kwakuwa hawalipwi mshahara.
.
Maamuzi yaliyopitishwa ilikua ni kila Shirikisho kupatiwa 100,000 USD ambazo katika mgawanyo huo imeelekezwa Rais wa kila Shirikisho atapatiwa 20,000 USD,Maendeleo Soka la Vijana 50,000 USD na kiasi cha 30,000 USD kusaidia tahadhari kwa Waamuzi.
.
Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia baada ya mgawo huo kuingia aliuelekeza kutumika kwa shughuli mbalimbali za Shirikisho, Hivyo basi tunakanusha taarifa zote zinazomuhusisha Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia kuchukua fedha hizo licha ya kuwa zimepitishwa katika vikao halali vya CAF.
IMETOLEWA NA TFF
Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23