Baada ya kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer kuanza vizuri kama kocha wa muda na baadae wakudumu akiwa na Man United, sasa umefika wakati wa kukumbana na changamoto za matokeo mabovu baada ya kujikuta akipoteza game yake ya sita ya Man United katika game zake nane zilizopita akiiongoza timu hiyo.
Man United leo ikiwa ugenini kucheza dhidi ya Everton huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake uliyopita wa UEFA Champions League dhidi ya FC Barcelona, leo wamejikuta wakipokea kipigo cha 8 katika EPL msimu wa 2018/2019 baada ya kufungwa kwa magoli 4-0.
Everton ambao wanaonekana hawana cha kushinda wala kupoteza msimu huu kutokana na nafasi yao ya kucheza Europa League msimu ujao kuwa finyu, magoli yao yamefungwa na Richarlison de Andrad dakika ya 13, Gylf Sigurdsson dakika ya 28, Lucas Digne dakika ya 56 na Theo Walcott dakika ya 64.
Man United katika michezo yake nane ya hivi karibuni iliyopita akishinda game mbili na kupoteza sita, hizi ndio game zenyewe Everton 4-0 Man United, FC Barcelona 3-0 Man United, Man United 2-1 West Ham, Man United 0-1 FC Barcelona, Wolves 2-1 Man United, Man United 2-1 Watford, Wolves 2-1 Man United na game ya Arsenal 2-0 Man United.
Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23