Msanii wa muziki Kaka Jay amesema amefanya kazi nyingi za Kimuziki na wanasiasa lakini akiwapigia simu wanaishia kumkatia wakihisi atawaomba hela.
Kaka Jay ameiambia Ayo Tv na Millardayo.com amewaimbia wanasiasa wengi akiwemo Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamis Kigwangalla ambapo kutokana na utunzi wake wabunge wengi walibadilishana namba zake ili awatungie nyimbo.
“Si unajua siasa za Kibongo mbunge ukishamfanyika kazi ukimpigia simu anahisi kama unataka kumtoboa kumbe ni salamu tu,“amesema.