NMB ikiwa ni benki ya chaguo la watanzania wengi jana Machi 19 ilifungua rasmi tawi lake jipya maeneo ya Sinza Mori mkabala na kituo cha kuwekea mafuta cha Big Born ikiwa na lengo la kuwafikia wateja wake.
Kwa sasa takribani zaidi ya wateja 300 wamekuwa wakihudumiwa kila siku katika tawi hilo ambalo limeanza kufanya kazi hivi karibuni ambapo limeonekana kuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi Sinza ikiwa ni moja kati ya maeneo yenye wakazi wengi jijini Dar es salaam.
Hii pia itakua inawahusu pamoja na wakazi wa mitaa jirani kama,Kijitonyama,Mabatini, Afrikasana,Tandale,Sayansi na maeneo mengine kwa kupata huduma za kibeki kwa uharaka zaidi.
Akizungumza katika ufunguzi huo Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam Bw.Salie Mlay amesema lengo kubwa la kupeleka tawi hilo ni kuwapa huduma kwa ukaribu wateja wao waliopo katika eneo hilo.
Amefafanua kuwa tangu kuanzishwa kwake tawi hilo limekuwa ni mkombozi kwa wateja wengi wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na watu mbalimbali >>’Tawi letu linatoa huduma zote za kibenki na tunazidi kuwakaribisha wateja wetu ili wajionee huduma bora zitolewazo na benki yetu na pia tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo za Mashine za kutolea fedha(ATM) ambayo hufanya muamala kwa masaa 24’.
Ufunguzi wa tawi hili la Sinza unafanya idadi ya matawi yaliyopo Kanda ya Dar es Salaam kufikia ishirini na tatu na kuifanya NMB kuendela kuwa benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania.
Tawi hili linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa NMB kama mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu,kufungua akaunti, kuweka na kutoa fedha nk, pia litakua linafunguliwa Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni ( 2:30 asubuhi – 10:30 jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (2:30 asubuhi- 6:30 mchana), Jumapili na siku za Sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi hili.