Hii ni Taarifa mbaya ni taarifa ya kifo cha moja kati ya mashabiki walioenda uwanjani kwa ajili ya kushuhudia mechi iliyokuwa ikichezwa kati ya Azam na Yanga uwanja wa Taifa Dar March 19.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma salaam zake za taarifa hii ambayo wanasema wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha shabiki Deodatus Mwakyangula kilichotokea Machi 19 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wataalam wa Tiba ya Wanamichezo Tanzania [Tasma] na Mjumbe Kamati ya Tiba Tff Dokta Ally Nassor Matuzya ameongea na millardayo.com na kuthibitisha kifo hicho na kusema>>’Tulipata taarifa za mtu ambaye amedondoka kutoka kwenye jukwaa la upande wa Mashariki wa uwanja wa taifa’
‘Wahudumu wa huduma ya kwanza walienda kumchukua wakamleta katika zahanati ya kwetu hapa uwanja wa taifa,tulimtambua kwa jina Deodatus Isaya Mwakyangula ana umri wa miaka 48 jina ambalo alituambia mkewe na kusema alikua mkazi wa Mkunguni A na meneja wa Rose Hill bar iliyopo Segerea’
‘Inasemekana baada ya goli la timu ya Yanga kuingia alisimama na kushangilia baada ya kukaa alionekana kuishiwa nguvu na kumlalia mkewe ambaye alienda nae kwenye mechi ile,baada ya muda mkewe alimuona anazidi kunyong’onyea alipojaribu kumpush kidogo kwa sababu za kishabiki alionekana amekwenda pembeni akitoa mapovu na kupoteza fahamu’
‘Mkewe aliomba msaada kwa majirani waweze kumsaidia na kuita watu wa huduma ya kwanza na kumleta kwenye kituo cha tiba hapa Uwanja wa Taifa,hali yake kiafya baada ya vipimo vilionyesha viko chini kabisa’
‘Vipimo vilionyesha hali ya uhai ilikua ndogo sana kwa kuwa uwanjani hatukua na vipimo vya kuthibitisha kwa pale uwanjani ndio tukaamua tumpeleke hospitali ya rufaa Temeke ambapo baadae ilitoka taarifa kuwa amefariki dunia’.
‘Kwa Uwanja wa Taifa sio mara moja wala mara mbili ni zaidi maana mechi nyingi zenye hamasa maana kwa sasa ushindani umeongezeka na ushabiki umeongezeka pia haya matukio yamekua yakitokea mara kwa mara’.