Baada ya kuzuka kwa kashfa kuwa club ya Simba SC imeifunga Mbeya City kwa upendeleo wa muamuzi wa mchezo huo, Afisa habari wa Simba SC Haji Manara leo kutokea jijini Mbeya aliongea na waandishi habari na kukanusha taarifa hizo kwa vigezo alivyo ita ni fact.
Kocha wa Mbeya City Ramadhani Nswazurimo alisema Simba SC wameshinda sababu ya kuwa na pesa akilalamikia kuwa wameshinda mchezo huo kutokana na refa kuwapa faulo aliyoidai ni nyepesi iliyopelekea Simba SC kupata goli la pili dakika ya 84 kupitia kwa Meddie Kagere katika ushindi wa 2-1.
“Muulizeni timu gani ya Burundi imewahi kuingia hatua ya makundu, sisi tumekwenda robo fainali ya CAF Champions League, anasema ndio maana mpira wa Tanzania hauendelei, je Burundi imewahi kupata timu hatua ya makundi”>>> Haji Manara
“Hakuna wa kutuzuia sisi kuwa Mabingwa halafu Mbeya City msivae ngoma wanayocheza Yanga Afrika wao wenyewe wameshindwa wameruka ukuta wamepita huku kule na tumewafunga, mbona Kagera hajavaa Mask hajaruka ukuta na ametufunga halafu sisi ukifanyahizo mbwembwe za kuruka ukuta lazima tukupige”>>>>Haji Manara
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania