Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewahakikishia Watanzania kuwa wizara yake imejipanga kutoa ufafanuzi wa maeneo yote ambayo yanapaswa kuwemo katika taarifa ya IMF ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ikiwemo utelezaji wa miradi mikubwa ya kiuchumi.
“Ili uchumi wa nchi ukue ni lazima uwe unawekeza, na bahati nzuri sana Mhe. Rais amemueleza mgeni wake jinsi tunavyowekeza kwenye miundombinu hususani ujenzi wa reli ya kati, jinsi tunavyowekeza katika ujenzi wa bwawa kubwa litakalotupatia megawati 2,100 za umeme na pia miradi ya barabara na viwanda vingi vilivyojengwa, haya ndio yanayokuza uchumi na sisi tunaamini kabisa wenzetu hawakuyazingatia kabisa katika taarifa ya awali (iliyovuja)” Dkt. Mpango.