Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amelizungumzia tukio la picha zinazoenea mitandao ya kijamii zikionyesha mtu anayefanya tendo la ngono ambapo anaonekana ni Askofu Gwajima ambapo ilielezwa kuwa angeitwa Polisi kwa ajili ya kuhojiwa.
Kamanda Mambosasa amesema baada ya Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi amesema Gwajima si mtuhumiwa bali ni muathirika wa tukio ambalo katika hali ya kawaida mtu yeyote asingetegemea lifanyike kutokana na kazi anayoifanya.
KAMANDA MAMBOSASA “TUTAMKAMATA ASKOFU GWAJIMA, TUMEONA, ULE NI UNYAMA”