Balozi wa Star Times Dina Marios ameendelea kutembelea shule za msingi jijini Dar es Salaam, ikiwa ni katika kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili ikiwa ndio chaneli ya kwanza ya katuni ya Kiswahili Tanzania.
Jumatano hii ilikuwa ni zamu ya Shule ya Msingi Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam ambapo wawakilishi hao walikutana na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la 3 na 4 kutoka shule hiyo.
Mbali na kuzungumza na wanafunzi walitoa zawadi kwa ya king’amuzi cha Dish kwa uongozi wa shule na zawadi kadha wa kadha kwa wanafunzi waliojibu vizuri maswali na wale wanaofanya vizuri darasani.
“Tunashukuru sana kwa ugeni huu wa StarTimes kuja shuleni kuzungumza na wanawafunzi na kuwapatia chachu ya kujifunza zaidi na kuwasaidia kupata msukumo wa kufanikiwa kwenye masomo yao”, alisema Mwl. Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Mchikichini Amani Levison Kidiala.
“Pia maudhui ya chaneli hii yamewachangamsha wanafunzi na pia itakuwa ni sehemu ya ukuaji wao kwa sababu kuna vitu vingi wanavyoweza kujifunza kupitia vipindi ambavyo vinafundisha sanaa na stadi mbali mbali za kimaisha.” Aliongeza.
ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambay wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao.
“Vipindi vingine vina mafunzo ya ustadi ambao utawasaidia watoto kujijijenga kiakili na kujiamini zaidi. Lengo letu kuja shule ya Mchikichini ni kwa sababu wanafunzi wa shule hii wanabeba uhalisia wa watoto wengi wa kitanzania”. Zamaradi Nzowa Meneja Maudhui, StarTimes Tanzania.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania