Alhamisi hii Dina Marios ambaye ni balozi wa Star Times alitembelea shule ya Msingi Makuburi Jeshini iliyoko Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo wwalikutana na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la awali hadi darasa la nne kutoka shule hiyo.
Pamoja na kuzungumza na wanafunzi wawakilishi wa StarTimes walitoa zawadi kwa ya king’amuzi na Dish kwa uongozi wa shule na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi walioweza kujibu vizuri maswali yaliyoulizwa.
“Asanteni sana kwa kututembelea Shuleni kwetu na kwa zawadi mlizotuletea sisi pamoja na wanafunzi. Mmewapa changamoto wanafunzi wetu lakini pia mmetuonyesha ni wapi tunahitaji kuongeza juhudi katika ufundishaji kwa sababu hapa tumeona watoto wanaelewa zaidi kwa kutazama kama wanavyojifunza kupitia maudhui ya chaneli yenu ya ST Kids.” Mwl. Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Makuburi Jeshini Bi. Mary Antony Manyika.
ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambayo wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao.
“Lengo letu kutembelea shule hizi ni kutambulisha maudhui mapya yanayopatikana katika chaneli ya ST Kids ambayo yako katika lugha ya Kiswahili. Vipindi ni vizuri kwa watoto kwani vinawafundisha stadi mbali mbali za maisha.” Dina Marious Balozi wa StarTimes Kids
Kampeni hii ya kutembelea mashule jijini Dar es Salaam itaendelea hadi mwisho wa mwezi wa tano na itafikia jumla ya shule 7 katika Wilaya 3 za Mkoa wa Dar es Salaam
Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC