Waziri mkuu Tayyip Erdogan wa Uturuki amezungumza katika mkutano wa hadhara wa uchaguzi kwamba anataka kuuondoa mtandao wa kijamii wa twitter katika nchi hiyo bila ya kujali mawazo ya jumuiya ya kimataifa tarehe 20 March 2014 ambapo Serikali hiyo ilifunga akaunti milioni 12 za raia wa Uturuki.
Sababu iliyotolewa juu ya kitendo hicho kutoka kwa ofisi ya waziri mkuu ni kwamba kuna ongezeko la kesi za wananchi wa Uturuki kuhusiana na twitter kila siku na kuna uwezekano sababu yenyewe hasa ikawa ni tofauti kwasababu Erdogan amekua akikasirishwa na uvujaji wa rekodi za mazungumzo yake ya simu kwenye mtandao huo.
Amezungumza na familia, Wanachama wa baraza la mawaziri, Waandishi wa habari na mazungumzo ya kibiashara pia malalamiko ya utumiaji wa rushwa juu yake ambapo hii imeanza tangu Disemba 17 2013 wakati ufisadi ulianza kutambulika katika nchi hiyo na kusababisha kujiuzulu kwa Mawaziri wanne mpaka sasa.
Badala ya kufungua uchunguzi Mahakamani juu ya tuhuma hizi za rushwa, Erdogan amekua akilaumu majaji, waendesha mashtaka, Polisi na mitandao ya kijamii kujaribu kumpindua baada ya kuwa wanatumiwa na aliekua mshirika wake wa karibu Fethullah Gulen wa marekani.
Wakati Uturuki inaelekea kwenye uchaguzi march 30, Erdogan na wasaidizi wake wa karibu wamekuwa wakiogopa kutokezea kwa uvujaji wa habari za ndani ambao utaweza kuathiri cheo cha chama tawala .
Hakukua na mategemeo ya yeye kuchukua sheria ya kufunga mtandao wa kijamii wa twitter haraka kama alivyofanywa lakini pia saa kadhaa baada ya kufungwa na kupigwa marufuku kwa mtandao huo, wananchi wa Uturuki wameweza kurudi twitter kupitia teknolojia ya digital.
Kati ya raia waliorudi twitter baada ya kufungwa huko kwa mtandao ni naibu waziri mkuu Bulet Arinc na Meya Melih Gökçek wa nchi hiyo ambae anafahamika kuwa mtumiaji mkubwa wa mtandao huo.
Pia raisi Abdullah Gül ambaye alipitisha sheria hiyo naye aliivunja baada kusema kupitia twitter kwamba hajaikubali sheria hiyo lakini pia mshirika muanzilishi wa mtandao wa kijamii wa twitter, Jack Dorsey alituma tweet akishauri watumiaji wa uturuki kutumia simu kwa njia ya ujumbe yaani message.
Dosey aliretweet post iliyotumwa na twitter’s global policy team ( timu ya sera za uma za kimataifa ya twitter) iliyosema watumiaji hao watumie ujumbe kwa kuanza na neon START na kutuma kwenda namba 2444, pamoja na 255.