Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayeichezea club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta amefanikiwa kurudi Tanzania salama akitokea Ubelgiji, Samatta amewasili Tanzania akiwa ametoka kuisadia KRC Genk kutwaa Ubingwa wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Ubelgiji baada ya miaka nane kupita.
Samatta baada ya mafanikio hayo tayari watu wameanza kuuliza kuhusiana na mipango yake ya siku za usoni kama ataendelea kuichezea KRC Genk katika msimu wa 2019/2020 au ndio anaanza safari mpya kwenda Ligi Kuu England kukamilisha ndoto yake ya kupata nafasi ya kuvichezea vilabu vya huko.
“Huwezi kujua kinachokuja mbeleni lakini mimi siku zote tulishakuwa tunaenda kwenye mabanda ya mipira watu wengi wanayajua, mimi nilikuwa mmoja wao kwenda kuangalia Ligi Kuu ya Uingereza kitu ambacho kilikuwa kinanivutia sana, napenda kwenda kucheza Ligi Kuu ya Uingereza lakini huwezi jua kila kitu kitakachokuja mbele ila tunahisi kitakachokuja”>>>Samatta
EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega