Leo May 30, 2019 nakusogezea stori kutoka DR Congo ambapo Mwili wa aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini, Etienne Tshisekedi ambaye ni baba wa Rais Felix Tshisekedi utawasili leo nchini DRC baada ya kuhifadhiwa kwa miaka miwili nchini Ubelgiji.
Tshisekedi alifariki mjini Brussels akiwa na miaka 84, February 2017 lakini mwili wake ulisalia Ubelgiji kutokana na wasiwasi wa kisiasa.
Tangu Tshisekedi afariki dunia wakati wa utawala wa Joseph Kabila, familia ya Tshisekedi ilikuwa ikivutana na Serikali wakati huo kuhusu mahali ambapo mwili wake utazikwa hali iliyosababishwa kuchelewesha kuurejesha mwili wake.
LAZARO NYALANDU AFUNGUKA MWANZO MWISHO ALIVYOKAMATWA “WALITUVAMIWA NA BUNDUKI”