Baada ya kuonekana kuwa na uwezekano mdogo wa kuendelea kufundisha Stamford Bridge kwa kudaiwa kuwa mmiliki wa timu hiyo Roman Abramovich hajapenda mwenendo wa timu hiyo, kocha Maurizio Sarri anaonekana kuwa na bahati.
Mtandao wa daily mail umeripoti kuwa Maurizio Sarri aliyejiunga na Chelsea akitokea Napoli 2018, sasa yupo mbioni kurejea Italia na kuendeleza kazi yake ya ukocha baada ya kudaiwa kumrugenzi wa Juventus Fabio Paratici anafanya mazungumzo na Chelsea, Sarri inaripotiwa kuwa yupo mbioni kurejea Italia ila safari hii katika club ya Juventus ya Italia.
Ili afanikiwe kuvunja mkataba wake na Chelsea itahitajika pound milioni 7 tu, Chelsea kwa sasa wanadaiwa kutaka kumrejesha kiungo wao wa zamani Frank Lampard kwa ajili ya kuifundisha club hiyo kama mbadala wa Maurizio Sarri ila hawataki kumtimua moja kwa moja kwa sababu wanaamini ana ofa na hawataki walipe fidia zaidi ya kutaka kufaidika na dili lake la Juventus.
EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega